You are currently viewing MSANII WA KIKE KUTOKA KENYA VIVIAN AKIRI KUPITIA MAGUMU KIMAISHA

MSANII WA KIKE KUTOKA KENYA VIVIAN AKIRI KUPITIA MAGUMU KIMAISHA

Msanii wa kike nchini Vivian anaendelea kufunguka kuhusu maisha yake ya ndani, amedai kwamba katika kipindi cha miezi 6 iliyopita amekuwa kwenye hali ngumu kimaisha.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Vivian amesema wiki hii iliyopita ndio mambo yalianza kumuendea murama huku akidai kuwa amepoteza imani kabisa kwenye upendo wa kweli kwani alivunjwa moyo na kuumizwa vibaya jambo ambalo amedai limemuacha hoi.

Haikushia hapo mrembo huyo alienda mbali zaidi na kusema kwamba amekuwa akitia bidii kuhakikisha kwamba kila kitu kinaenda sawa huku akisisitiza kuwa ana imani mambo yatakuwa mazuri hivi karibuni kwani anaamini dunia itampa nafasi tena ya kujipenda mwenyewe.

Hata hivyo Vivian hajaweka wazi kinachosumbua maishani ila ujumbe wake umeibua maswali mengi miongoni mwa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ambapo wengi wamehoji kuwa huenda ndoa ya Vivian na mume wake Sam West imeingiwa na ukungu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke