Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Vinka, ametangaza mpango wa kuja na tamasha la muziki ndani ya mwaka huu wa 2022.
Vinka ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Fimbo amethibitisha hilo kwenye moja ya performance yake huko Munyonyo nchini Uganda wikiendi iliyopita ambapo amesema onesho hilo ni kwa ajili ya kusherekea miaka 5 ya uwepo wake kwenye muziki pamoja na mashabiki zake.
Hata hivyo msanii huyo wa Swangz Avenue hajaweka wazi ni lini hasa atakuja na onesha lake la muziki ila ni jambo la kusubiriwa.
Utakumbuka Vinka alianza safari ya muziki chini lebo ya muziki ya Swangz Avenue mwaka wa 2017 alipoachia singo yake ya kwanza iitwayo Levels ikafuatwa na Stylo aliyomshirikisha bosi wake wa zamani Irene Ntale.
Tangu kipindi hicho amekuwa na muendelezo wa kuachia nyimbo kali bila kupoa jambo ambalo limempelekea kushinda tuzo nyingi nchini Uganda lakini pia imempelekea kuingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya Sony Music, tawi la Afrika.