Aliyekuwa msanii wa Junge Masters Lypso amefariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 17, 2022 kaunti ya Nairobi.
Taarifa hiyo imethibitisha na rafiki yake wa muda mrefu Dogo Richie ambaye amesema msanii huyo alianguka ghafla akiwa bafuni na kufariki papo hapo.
Kwa mujibu wa Dogo Richie mipango ya kumpumzisha Lypso kwenye nyumba yake ya milele inaendelea huku akiwataka mashabiki kuiweka familia yake kwa maombi wakati huu mgumu.
Lypso ambaye amemuacha mke na mtoto mmoja, enzi za uhai wake aliwahi kutamba na nyimbo kama Size Yangu, Samantha na nyingine nyingi.