Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar hatashiriki mechi mbili zijazo za Brazil za Kombe la Dunia (Switzerland & Cameroon) baada ya kupata jeraha sehemu ya fundo la mguu wa kulia, kwa mujibu wa taarifa toka kwa daktari wa timu yao.
Mshambuliaji huyo aliondolewa uwanjani dakika ya 80 ya mchezo wa siku ya Alhamisi ambapo Brazil waliichapa Serbia 2-0 baada ya kukabiliwa vikali na Nikola Milenkovic.
Hivyo Neymar anatarajiwa kurejea uwanjani katika hatua ya mtoano ikiwa Mabingwa hao mara 5 wa kombe la Dunia watafuzu kwenda hatua hiyo