Mshukiwa wa mauaji ya Rapa Young Dolph, Shundale Barnett ameachiwa huru kutoka Jela. Barnett ameachiwa kwa dhamana baada ya maafisa wa jeshi nchini Marekani kusema hakuwa na hatia, na alikuwa nyuma ya gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na mshukiwa namba 1 wa mauaji hayo, Justin Johnson.
Young Dolph alipigwa risasi Novemba 17 mwaka 2021 akitoka kununua cookies kwenye duka moja mjini Memphis Tennessee. Uchunguzi unaeleza muuaji alifika katika duka hilo na kushuka kwenye gari aina ya Mercedes Benz kisha kumfyatulia risasi kadhaa Dolph hadi umauti ukamfika.