Kama kuna kitu ambacho Mchekeshaji Eric Omondi anajivunia kuwa nacho ni kujiamini, baada ya jaribio lake la kwanza la kuikingia kifua muziki wa kenya kutibuka na hata kupelekea kukamatwa kwake, mchekeshaji huyo Hatimaye amewasilisha mswada bungeni kutaka muziki wa Kenya upewe hadhi.
Mswada huo umepokelewa na wabunge Babu Owino wa Embakassi Mashariki na mwenzake Charles Njagua wa Starehe. Wabunge hao wameapa kuhakikisha mswada huo unapitishwa bungeni huku wakitoa wito kwa wasanii wa Kenya kutoa muziki mzuri wenye maudhui safi.
Akizungumza baada ya kuwasilisha mswada huo bungeni Omondi amewatolea uvivu wasanii waliodhani mpango wake wa kutetea muziki wa Kenya utafeli huku akiwataka wasanii wa Kenya wajenge tabia ya kuwa na umoja wanapokuwa wanatetea maslahi yao.
Hata hivyo mswada huo wa Eric Omondi wa kutaka asilimia 75 ya muziki zipigwe kwenye vituo vya redio na runinga nchini utawasilishwa leo bungeni na wabunge Babu Owino na Charles Njagua