Prodyuza Motif Di Don amefunguka mpango kuachana kabisa masuala ya kutayarisha muziki na badala yake kugeukia usanii wa kuimba nyimbo.
Kwenye mahojiano na SPM Buzz Don amesema mwakani atazindua rasmi kazi zake kama mwimbaji huku akidai kuwa amejipanga kuanza safari yake mpya kwenye muziki.
Prodyuza huyo amesema mwaka 2022 hajakuwa akionekana sana akitayarisha nyimbo za wasanii wa muziki nchini kwa sababu alikuwa amejikita zaidi kuboresha ustadi wake kwenye masuala ya uimbaji.
Kauli ya Motif Di Don imekuja siku moja baada ya kutoa changamoto kwa watayarishaji wa muziki kubuni sauti mpya ya muziki wa kenya kwa ajili ya kuleta ushindani kwenye soko la kimataifa.
Hata hivyo alienda mbali na kumtaka prodyuza ambaye ataunga mawazo yake awasiliana naye ili waifanyie kazi pendekezo hilo.
Utakumbuka Motif Di Don ni muasisi wa muziki wa gengetone ambao umepata umaarufu nchini lakini pia unatajwa kuwa ndio utambulisho wa muziki wa kenya kimataifa.