You are currently viewing MTAYARISHAJI WA VIDEO SASHA VYBZ AANIKWA KWA KUMUADA FRESH KID

MTAYARISHAJI WA VIDEO SASHA VYBZ AANIKWA KWA KUMUADA FRESH KID

Miaka miwili Fresh kid alipata umaarufu kwenye muziki wake na akaiteka tasnia ya muziki nchini Uganda kwa kishindo.

Rapa huyo mchanga alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki mzuri na nyimbo zake jambo ambalo lilimpelekea kuanza kuingiza pesa kupitia kazi zake.

Mwaka wa 2019 serikali ya uganda iliingia kati na kumtaka Fresh Kid aache muziki na aelekeze nguvu zake kwenye masomo yake.

Waziri Nakiwala Nakinyingi alimuagiza asitishe shughuli za kurekodi nyimbo zake ambapo alilazimishwe aachie wimbo wake uitwao Bambi bila video.

Sasa kuonyesha kwamba anamjali sana Fresh Kid, Mtayarishaji video nchini Uganda Sasha Vybz alimuahidi kusimamia gharama zote za kuandaa video ya wimbo wa Bambi, singo ambayo ilitayarishwa na studio zake za Savy Filmz.

Lakini cha kusikitisha hadi sasa Sasha Vybz hajatimiza ahadi aliyotoa kwa Fresh Kid jambo ambalo limewafanya watumiaji wa mitandao ya kijamii kumshambulia mtayarishaji huyo wa video kwa madai ya kutoa ahadi ya uongo kwa rapa huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke