Muigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani Stacey Dash amezua maswali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuibuka na kudai kuwa hakuwa anajua kama rapa DMX amefariki.
Kupitia video ya tiktok aliojirekodi muigizaji huyo amesema kuwa amepata taarifa za rapa huyo kufariki siku ya Jumatano ya Agosti 31, mwaka 2022 tangu rapa huyo afariki April 9,mwaka 2021,
Kupitia ukurasa wake wa instagram ameshare video hiyo yenye majonzi tele na kuisindikiza na ujumbe uliokuwa ukilaani sababu zilizopelekea kifo cha rapa huyo.
“Sikujua kama DMX alikufa,” “sikujua, ni kutokana na kuzidisha madawa ya kulevya . mimi leo, nina miaka sita na mwezi mmoja nipo safi, na inanivunja moyo. inavunja moyo wangu kwamba alipoteza. alishindwa na pepo huyo .” Ameandika