Muigizaji nyota wa series ya “Squid Game” O Yeong-su amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono.
Kulingana na ripoti za ndani, muigizaji huyo amefunguliwa mashtaka bila kutiwa kizuizini kwa madai ya kutomasa mwili wa mwanamke vibaya mwaka 2017 huku mwenyewe akidai alimshika mkono kumuelekeza njia.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 78, ambaye amejulikana zaidi kupitia series hiyo ya Squid game iliyopata umaarufu mkubwa Netflix ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kutoka Korea Kusini kushinda tuzo ya Golden Globe.