Mchekeshaji Kendrick Mulamwah ametangaza ujio mpya wa msanii wake val wambo ambaye yupo chini ya lebo yake ya muziki ya Mulamwah Ent.
Kwenye mahojiano na podcast ya VIncent Mboya, Mulamwah amesema msanii wake huyo kwa sasa yupo chimbo anaanda ep yake mpya, hivyo mashabiki zake watarajie muziki mzuri kutoka kwake.
Mulamwah aidha amebainisha kuwa hana mpango wa kumsajili msanii mwingine kwenye lebo yake kutokana na changamoto ya kifedha.
Ikumbukwe mapema mwaka huu val wambo alitambulishwa chini uongozi wa mulamwah ent na amefanikiwa kuachia nyimbo tatu ambazo ni Umenilemea na Serereka akiwa ammshirikisha Ruth K.