You are currently viewing MULAMWAH ATISHIA KUMSHTAKI BABY MAMA WAKE CAROL SONNIE

MULAMWAH ATISHIA KUMSHTAKI BABY MAMA WAKE CAROL SONNIE

Mchekeshaji Mulamwah ametishia kumchukulia hatua kali za kisheria Baby Mama wake Carol Sonnie kwa hatua ya kumtumia vibaya mtoto wao mtandaoni.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mulamwah ametoa ya moyo kwa kusema kuwa amechukizwa na kitendo cha Baby mama wake huyo kumtumia mtoto wao kama kitega uchumi, jambo ambalo amedai kuwa si cha kingwana kwani amekiuka haki ya faragha ya mtoto wao.

Mchekeshi huyo ameenda mbali zaidi na kwa kudai kwamba kinachomuuma zaidi ni hatua ya mrembo huyo kumzushia madai ya uongo kwenye vyombo vya habari kuwa kuna kipindi alimshushia kichapo cha mbwa akiwa mja mzito, madai ambayo Mulamwah ameyakanusha vikali.

Mapema wiki hii Mulamwah na Baby Mama Carol Sonnie walitupiana maneno makali mtandaoni kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwa mtoto wao baada ya mchekeshaji huyo kudai kuwa mzazi mwenzie amekuwa akimpa wakati mgumu kwenye suala la kutoa matunzo kwa binti yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke