You are currently viewing Mume wa Cindy Sanyu akanusha tuhuma za kushindwa kufadhili harusi yao

Mume wa Cindy Sanyu akanusha tuhuma za kushindwa kufadhili harusi yao

Mwanamuziki Cindy Sanyu na mumewe, Prynce Okuyo juzi kati walitimiza mwaka mmoja wakiwa mke na mume baada ya kufanga ndoa mwishoni mwa mwaka 2021.

Kufuatia uvumi kuwa Cindy ndiye alifadhili shughuli nzima ya harusi yao, mume wake Prynce Okuyo amejitokeza kwa mara ya kwanza na kukata mizizi ya fitina juu ya madai hayo.

Okuyo ameeleza kuwa aliwekeza pesa zake nyingi kwenye harusi yao lakini pia alipokea michango kutoka kwa marafiki wao.

“Je, uliona risiti yoyote kutoka kwake akikwambia alifadhili harusi pekee yake. Niliwekeza mamilioni ya pesa kuona hafla hiyo inafanikiwa. Hata marafiki zetu walitoa mchango mkubwa,” alisema katika mahojiano na televisheni moja nchini Uganda.

Mpiga picha huyo pia alikanusha tuhuma za kulelewa na Cindy katika ndoa yao kwa kusema kuwa anatekeleza majukumu ya familia kama mume.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke