Mume wa marehemu Osinachi Nwachukwu, amekamatwa kufuatia kifo cha mwimbaji huyo wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria.
Msemaji wa polisi mjini Abuja amenukuliwa na tovuti za Daily Trust and Punch akithibitisha kukamatwa kwa Peter Nwachukwu baada ya malalamiko kutoka kwa kaka ya mwimbaji huyo.
Kukamatwa kwa Peter Nwachukwu kumukuja mara ya baada tetesi kusambaa mitandaoni kuwa huenda kifo cha mwimbaji huyo kulitokana na kupigwa na mume wake.
Osinanchi, alifariki siku ya Ijumaa katika hospitali ya mji mkuu, Abuja
Itakumbukwa, Marehemu Osinachi alipata umaarufu mwaka 2017 kwa wimbo wake uitwao “Ekwueme” aliouimba na Prospa Ochimana.