Mrembo maarufu mtandaoni Vera Sidika amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kukiri hadharani kufanyiwa upasuaji wa kupunguza makalio yake baada ya kuona anapata matatizo kiafya.
Mama huyo wa mtoto mmoja Vera amedai kupitia kipindi kigumu katika safari hiyo ya kubadilisha mwili wake huku akiwashauri wanawake kutojaribu kufanya upasuaji wowote wa kuongeza au kupunguza kitu miili yao kwani itawaletea shida huko mbeleni..
“Wanadada tafadhalini, mjue kujipenda mlivyo na msikubali shinikizo la rika liwafanye mkimbilie kufanya mambo ambayo yatawaharibia maisha yenu huko mbeleni,” alisema kupitia Instagram.
Ikumbukwe kuwa mrembo huyo kutoka Kenya amewahi kushare picha akiwa na muonekano wa rangi nyeusi, jambo ambalo lilichukuliwa na wengi kama kiki baada ya kubainika kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli.