Nyota wa muziki nchini Nadia Mukami anadaiwa kushika ujauzito wa mpenzi wake Arrow Boy
Uvumi huo umeanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na muendelezo wa picha na mavazi ambayo Nadia Mukami amekuwa akivaa kwa sasa.
Kwanza kabisa ni picha aliyopiga na Arrow Boy ambayo inamuonesha Nadia Mukami kuficha tumbo lake mbele ya camera jambo ambalo si kawaida yake.
Haijaishia hapo, vazi ambalo Nadia Mukami alilivaa juzi kati akimsuprise mpenzi wake Arrow Boiy uraiani baada ya kutoka hospitali limefanya watu kupigia mstari kuwa mrembo huyo ni mjamzito kwani alikuwa amevaa nguo kubwa (Oversize)
Ikiwa ni kweli Nadia Mukami ana ujauzito kwa sasa, basi huyo atakuwa mtoto wa kwanza kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 26 na mchumba wake Arrow Boy