You are currently viewing MUUNGANO WA WANAMUZUKI UGANDA KUFANYA UCHAGUZI KWA NJIA YA MTANDAO

MUUNGANO WA WANAMUZUKI UGANDA KUFANYA UCHAGUZI KWA NJIA YA MTANDAO

Muungano wa wanamuziki nchini Uganda ambao unajiandaa kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya mwezi huu wa Aprili umesema utafanya uchaguzi huo kwa njia ya mtandao.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Rais wa Muungano huo Cindy Sanyu amesema wamechukua hatua hiyo kwa sababu hawana fedha za kutosha kufanya uchaguzi kwa mfumo wa kawaida ambao unatoa nafasi kwa wanachama wao kupiga kura moja kwa moja kwa kujiwasilisha wenye kwenye vituo vya kupigia kura.

“Fedha nyingi inahitajika kuandaa uchaguzi kwa njia ya kawaida na kwa sasa hatuna pesa za kutosha,” alisema Cindy.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Local Man” amesema muungano wa wanamuziki nchini Uganda umekosolea vibaya na wasanii kwa hatua yake ya kuendesha uchaguzi kwa njia ya mtandao huku akieleza kuwa wana mpango wa kuandaa uchaguzi wa kawaida kama watapata pesa kutoka kwa wahisani.

“Ndio nafahamu watu wengi wanachukulia kupiga kura mtandaoni sio sahihi ila ndio njia pekee ambayo tuko nayo kwa sasa. Lakini ikitokea tumepata pesa kutoka kwa hisani na washirika wengine wa maendeleo, tutafanya uchaguzi kwa njia ya kawaida,” aliongeza Cindy.

Cindy Sanyu alichaguliwa kuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda mwezi Machi mwaka wa 2021 kujaza nafasi ya Ykee Benda ambaye alijiuzulu.

Utakumbuka Ykee Benda alichukua nafasi ya Sophie Gombya ambaye alijiuzulu pia na kujiunga na siasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke