Hali ya sintofahamu imezuka baada ya mwamuzi Janny Sikazwe kutoka nchini Zambia kumaliza mpira kabla ya wakati kwenye mchezo wa Kundi F kati ya Tunisia dhidi ya Mali.
Katika dakika ya 85 mwamuzi Janny alipuliza kipyenga kuashiria kumalizika kwa mchezo huo lakini baada ya vuta ni kuvute alibadili mawazo na kurejesha mchezo, lakini katika hali isiyo ya kawaida Janny Sikazwe alimaliza mpira tena katika dakika 89 na sekunde 43.
Hata licha ya kuvutana na viongozi wa timu ya Taifa ya Tunisia, Janny Sikazwe aliendelea kushikilia maamuzi yake na mechi hiyo ikamalizika kwa Mali kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Tunisia