You are currently viewing MWANAMKE ALIYEPEWA UJA UZITO NA MSANII WA SOL GENERATION BENSOUL AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA

MWANAMKE ALIYEPEWA UJA UZITO NA MSANII WA SOL GENERATION BENSOUL AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA

Mwanamke aliyebebeshwa uja uzito na msanii wa sol Bensoul amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya Bensoul kukiri hadharani kuwa alimsaliti mpenzi wake Noni Gathoni kwa kumpa uja uzito mrembo huyo kutoka Mombasa.

Kwenye kikao cha maswali na majibu na mashabiki kwenye mtandao wa instagram mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Tiffany amesema hakuwa na nia ya kuvunja uhusiano wa bensoul na mchumba wake kipindi alihamua kutoka  kimapenzi na msanii huyo ila ni jambo ambalo lilitokea bahati mbaya.

Mrembo huyo amekanusha taarifa zinazotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatumia jina la Bensoul kujitafuta kiki kwa kusema kuwa hana haja na umaarufu ikizingatiwa kuwa ni kweli ana uja uzito wa Bensoul.

Hata hivyo amempongeza Bensoul kwa kujitokeza hadharani na kukubali kuwa ana uja uzito wake kwani ni wanaume wachache ndio wana uwezo wa kufanya hivyo.

Kauli ya mrembo huyo imekuja mara baaada ya bensoul na mchumba wake noni Gathoni kuonekana wakionyeshana mahaba mazito kwenye mtandao wa instagram licha ya kuwa bensoul aliripotiwa kumsaliti mpenzi wake huyo kwa kumpa mwanamke mwingine uja uzito kwenye moja ya performance yake mwaka wa 2021 huko Mombasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke