You are currently viewing MWANAMKE MMOJA AJITOKEZA NA KUDAI KWAMBA NI MTOTO WA DMX

MWANAMKE MMOJA AJITOKEZA NA KUDAI KWAMBA NI MTOTO WA DMX

Vita ya urithi wa mali kwenye familia ya DMX inaendelea kushika kasi, wiki hii amejitokeza mwanamke mmoja na kudai kwamba ni mtoto wa marehemu DMX, hivyo kufanya namba ya watoto wake kufikia 15.

Kwa mujibu wa Page Six, wiki kadhaa zilizopita mwanamke huyo aitwaye Raven Barmer-Simmons alimtafuta mtoto mkubwa wa DMX na kumwambia kwamba yeye ni mtoto wa DMX.

Hata hivyo kwa mujibu wa mahakama watoto wote 14 akiwemo na mwanamke huyo watafanyiwa vipimo vya DNA kubaini uhalali wao kwa ajili ya kugawa urithi kwa usahihi.

Hii yote inatokana na kutoelewana kwa watoto wa DMX juu ya urithi wa mali zilizoachwa na mkongwe huyo wa Hip Hop ambaye alifariki dunia April 9 mwaka huu.

Mwishoni mwa juma lilopita Jaji aliwateua watoto watatu; Xavier, Tacoma na Sean Simmons kuwa wasimamizi wa muda wa mali za baba yao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke