Mwanamke mmoja jijini Nairobi kwa jina la Caro Leehavi ameibuka na kutishia kuanika wazi picha pamoja na video za utupu akila uroda na mchekeshaji Maarufu nchini Eric Omondi.
Hii ni baada ya mchekeshaji huyo kudaiwa kushindwa kuheshimu mkataba wao maelewano kati yake na mwanamke huyo ambao ulikuwa unamtaka Eric Omondi amlipe shillingi elfu 25 kabla ya mchezo kukamilika.
Akipiga stori na Plug TV mwanamke huyo ambaye ni mfanyibiashara jijini Nairobi amesema Eric Omondi alisepa baada ya tendo na akaishia kulimpa shillingi elfu moja ya nauli jambo ambalo anadai kuwa lilimtia hasira ikizingatiwa kuwa alikwenda kinyume na taratibu zake za maisha kwa kutoka kimapenzi na mchekeshaji huyo.
Licha ya mwanamke huyo kuibua tuhuma hizo dhidi ya Eric Omondi, mchekeshaji hajatoa tamko lolote kuhusiana na hilo ila ni jambo la kusubiriwa.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kupuzilia mbali tuhuma za mwanamke huyo wakidai kuwa amelimpwa na Eric Omondi kwa ajili ya kumtengenezea mazingira ya kuzungumziwa kwenye vichwa vya habari kwani mchekeshaji huyo anapenda sana maswala ya kiki.