You are currently viewing MWANAMUZIKI BAHATI KUWANIA URAIS NCHINI KENYA MWAKA 2037

MWANAMUZIKI BAHATI KUWANIA URAIS NCHINI KENYA MWAKA 2037

Staa wa muziki nchini Bahati ametangaza nia ya kugombea kiti cha Urais nchini Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2037.

Bahati ameyaweka wazi hayo mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akizindua azma yake ya kuwania ubunge wa mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu kwa kusema kuwa ana nia njema kwa wananchi wa Kenya kwani ana vigezo vya kutosha ya kuwa kiongozi atakayeleta mabadiliko nchini.

Hitmaker huyo wa ngoma “Adhiambo” amedai kwamba hana mpango wa kuacha muziki licha ya kwamba ametia nia ya kuomba ridhaa ya ubunge wa eneo la Mathare.

Lakini pia Bahati ameweka wazi mpango wa kuachia EP yake mpya mwezi Mei mwaka huu wakati atakapokuwa anaendeleza kampeini yake ya kujipigia debe kwenye azma ya kuwania ubunge wa Mathare.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke