Mwanamuziki kutoka nchini uganda Catherine Kusasira anadaiwa kuuza gari lake aina ya Land Cruiser V8 ambayo alizawadiwa na rais yoweri museveni baada ya kumteua kama mshauri wake.
Gari hilo limeripotiwa kuegeshwa kwa zaidi ya wiki moja kwenye mnada wa magari ya Pine uliyoko Nakasero, viungani mwa jiji la Kampala.
Ripoti zinaonyesha kuwa mwanamuziki huyo anaandamwa na madeni, hivyo Ameamua kuuza baadhi ya mali zake ili kuondokana na mzigo wa madeni.
Ikumbukwe Chanzo chake kikubwa cha mapato yalikuwa matamasha ya muziki lakini tangu yapigwe marufuku kutokana na janga la korona, hajakuwa na kitega uchumi dhabiti.