You are currently viewing Mwanamuziki Dolla Kabarry awashauri wanaume kujenga mazoea ya kuwapa zaadi wake zao

Mwanamuziki Dolla Kabarry awashauri wanaume kujenga mazoea ya kuwapa zaadi wake zao

Mwanamuziki wa Benga Dolla Kabarry ametoa changamoto kwa wanaume kujenga tabia ya kuwazawadi wake zao kama njia moja ya kupunguza vitendo vya usaliti kwenye ndoa.

Mwanamuziki huyo amesema wanawake wanapenda sana kupewa zawadi na wanaume wasipowajibika ipasavyo huenda jini mkata kamba akaingilia mahusiano yao.

Aidha amesisitiza kuwa sio lazima zawadi husika iwe ya gharama ya juu kama baadhi ya watu wanavyofanya mtandaoni ila kitendo cha kutoa zawadi kila mara ina nafasi kubwa ya kuwashawishi wanawake kutoshiriki vitendo vya usaliti.

Kauli yake inakuja mara baada ya kumnunulia mke wake gari mpya aina ya Toyota Harrier kama zawadi kwenye siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake Oktoba 17 mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke