Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Hopekid ameamua kutumia ipasavyo pesa ambazo anazitolea jasho
Hii ni baada ya kujizawadi gari aina Mercedes Benz kutokana na mafanikio ambayo ameyapata kupitia muziki wake.
Kupitia ukurasa wake instagram amechapisha picha ya gari yake mpya na kusindikiza na ujumbe unaosomeka “Allow me to celebrate my small wins with you ☺️😊☺️ let me bless ur TL with my brand new merc.”
Hata hivyo mashabiki pamoja na mastaa wenzake wamempongeza kwa mafanikio hayo huku wakimtakia kila la heri katika siku za mbeleni.