Mwimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya toka lebo ya Mavin Records nchini Nigeria, msanii Ayra Starr mwenye umri wa miaka 20, amejiunga rasmi na Golden Club ya Boomplay.
Hatua hiyo kubwa kwa Ayra Star inakuja baada ya streams zake zote za Boomplay kufika zaidi ya Milioni 100+ (100,000,000).
Hii inamfanya Ayra Starr kuwa msanii wa pili wa kike kutoka Nigeria kufikisha streams 100M+ baada ya Simi, lakini pia anakua msanii wa kike wa TATU kufikisha streams 100M+ Afrika. Namba moja ni Simi kutoka Nigeria, wa pili ni Zuchu kutoka Tanzania.
Utakumbuka, Ayra Star alitambulishwa rasmi kama msanii na lebo ya Mavin Records yake Don Jazzy mwezi Januari mwaka 2021 akiwa tayari amerekodi nyimbo tano ambazo ni ‘Away’, ‘Ija’, ‘DITR’, ‘Sare’ na ‘Memories’.