Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Lydia Jazmine amefunguka sababu za kutofanya vizuri kimuziki mwaka 2022.
Kwenye mahojano yake hivi karibuni amesema aliamua kuweka kila kitu pembeni kwa ajili ya kujitathmini na pia amekuwa akiendeleza biashara zake kimya kimya.
Mrembo huyo pia amedai kwamba mgogoro ulioibuka kati yake na uongozi wake wa zamani ulilemaza juhudi za kuupambania muziki wake.
Hata hivyo amesema mwaka 2023 anarudi na kishindo kwenye muziki wake kwani ana mpango wa kuachia nyimbo mfululizo bila kupoa.
Utakumbuka Lydia Jazmine alivunja mkataba na meneja wake wa zamani Ronnie Mulindwa kutokana na migogoro ya kifedha lakini kwa sasa anafanya kazi kwa ukaribu na prodyuza Bushingtone.