You are currently viewing MWANAMUZIKI LE GENERAL DEFAO AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 62

MWANAMUZIKI LE GENERAL DEFAO AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 62

Mwanamuziki mahiri wa Rhumba, Le General Defao Matumona amefariki  Desemba 27, 2021 akiwa na umri wa miaka 62 huko Douala, nchini Cameroon.

Mwanamuziki huyo mwenye kipaji cha kutunga na kuimba kwa sauti nyembamba na nyororo amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa nchini Cameroon.

Tovuti mbali mbali zimeeleza kwamba akiwa amelala masaa machache kuelekea onesho lake, Defao alipoteza fahamu kwa takribani masaa 4 akiwa katika chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia. Bado chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi.

Defao alizaliwa Desemba 03, mwaka 1958 katika jiji la Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na alianza kujishughulisha na muziki mwaka 1976, akiwa katika bendi ya Orchestra Suka Movema na baadaye akaenda kujiunga na bendi ya Fogo Stars.

Kando na Fogo Stars Defao alifanya kazi na bendi zingine kama Korotoro, Grand Zaiko Wawa, Choc Stars na Big Star bendi yake mwenyewe.

Katika kipindi cha uhai wake Defao alionesha ubunifu uliomletea mafanikio makubwa baada ya kufyatua album zisizopungua 17. Kati ya hizo, sita ziliingia katika soko la Ulaya mwaka 1995.

Wapenzi na mashabiki wake waliulinganisha umaarufu wake na ule wa wanamuziki kama Papa Wemba, Koffi Olomide, Bozi Boziana na Kester Emeneya na atakumbukwa na nyimbo kama Georgina, Fammilie Kikuta, Nadine, Bana Kongo, Oniva na Filie.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke