You are currently viewing MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI RWANDA YVAN BURAVAN AFARIKI DUNIA

MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI RWANDA YVAN BURAVAN AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki maarufu wa nchini Rwanda Yvan Buravan amefariki dunia, menejimenti yake imetangaza Kifo chake leo Jumatano August 17 kwamba amefariki kwa ugonjwa wa Saratani ya Kongosho akiwa nchini India alipokuwa akipokea matibabu tangu mwanzoni mwa mwezi huu.

Buravan ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 27, alianza Muziki mwaka 2009 lakini Afrika Mashariki ilianza kumuona mwaka 2015 alipoachia nyimbo zake kama ‘Urwo Ngukunda’ featuring Uncle Austin, ‘Malaika’, ‘Just a dance’ na nyingine kibao zikiwemo ‘Low Key’, ‘With You’, ‘Heaven’, ‘Bindimo’ na ‘Si Belle’ ambazo zilimpatia mafanikio makubwa

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke