You are currently viewing Mwanamuziki Ronald Alimpa asikitishwa na waliofuja pesa za kugharamia matibabu yake

Mwanamuziki Ronald Alimpa asikitishwa na waliofuja pesa za kugharamia matibabu yake

Msanii kutoka nchni Uganda Ronald Alimpa ameonesha kusikitishwa na kitendo cha msanii mwenzake Hassan Nduga kuhusika kwenye wizi wa pesa za msaada alizopewa na wahisani kwa ajili ya kugharamia matibabu yake.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Alimpa amesema  msanii huyo alifuja takriban shillingi millioni 1.5 kati ya millioni 2 alizopokea kutoka kwa msamaria mwema kwa kigezo cha kugharamia mahitaji ya wasanii wenzake waliopata naye ajali wiki moja iliyopita.

Hitmaker huyo huyo “Alimpa” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa licha ya Nduga kumsaidia kipindi alihusika kwenye ajali ya barabarani hajafurahishwa na kitendo chake cha kuwatangazia watu misaada aliyokuwa anampa akiwa hospitalini.

Utakumbuka Ronald Alimpa, Lady Grace na Ragga Fire walihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani huko Ssemuto Katika wiliya ya Nasakeseke wiki moja iliyopita, lakini kwa bahati mbaya  msanii lady grace alifariki dunia papo hapo huku akiwaacha wengine na majeraha mabaya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke