You are currently viewing Mwanamuziki wa Bongofleva H. Baba amtolea uvivu Harmonize kwa kumuiga Wizkid

Mwanamuziki wa Bongofleva H. Baba amtolea uvivu Harmonize kwa kumuiga Wizkid

Msanii wa Bongofleva H. Baba amedai kitendo cha Harmonize kumchagua Kajala kuwa Meneja wake ni matokeo ya kumuiga Wizkid ambaye mke wake, Jada P ndiye Meneja wake.

H. Baba amesema Meneja na mahusiano ni vitu viwili tofauti, huwezi kuvichanganya na kupata matokeo mazuri na pengine ndio sababu ya baadhi ya wasanii kuondoka Konde Music.

“Wanataka kuiga kwa Wizkid, hawawezi. Meneja au mke wa Wizkid alikuwa anamsimamia Chris Brown, kwa hiyo kuja kumsimamia Wizkid ni jambo jepesi kwa sababu ana uzoefu, sasa huyu dada yetu hana uzoefu wa hicho” amesema H. Baba.

Utakumbuka tangu Kajala Masanja amekuwa Meneja wa Konde Music, wasanii watatu, Cheed, Killy na Anjella wameachana na lebo hiyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke