You are currently viewing MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA KILLY KUACHIA THE GREEN LIGHT EP IJUMAA HII

MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA KILLY KUACHIA THE GREEN LIGHT EP IJUMAA HII

Mwanamuziki wa Bongofleva Killy ametangaza tarehe mpya ya kuachia EP yake ya The Green Light.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Killy amesema Ep hiyo Itatoka rasmi Februari 25 siku ya Ijumaa ikiwa na jumla ya nyimbo 6 za moto.

Msanii huyo wa Konde Gang amewaomba radhi mashabiki kwa kuisogeza mbele tarehe ya kutoka kwa EP hiyo ambayo ilipaswa kuachia Februari 20 mwaka huu kwa kusema kwamba kuna vitu havikuenda sawa kwa upande wake hivyo alilazimika kuahirisha shughuli ya kuachia The Green Light EP.

Katika EP hiyo Killy amemshirikisha christian bella katika wimbo namba 6 uitwao ‘Niambie’, Ibraah katika wimbo namba 3 uitwao ‘Kiuno’ na boss wake harmonize katika lead singo yake iitwayo “Ni wewe” ambayo tayari imekwisha toka.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke