You are currently viewing Mwanamuziki wa Cameroon atoa ya moyoni baada ya kuchoshwa na muziki wa Nigeria nchini kwao

Mwanamuziki wa Cameroon atoa ya moyoni baada ya kuchoshwa na muziki wa Nigeria nchini kwao

Baada ya kilio cha Wakenya na wana Afrika Mashariki kuhusu upigwaji wa nyimbo za Nigeria kukithiri kwenye kumbi za starehe na maeneo mbali mbali, hatimaye kilio hicho kimefika hadi kwa wana Afrika Magharibi wenyewe.

Kupitia mtandao wa Facebook, mwanamuziki wa Cameroon AmbeDiSing ameibuka na malalamiko ya kukithiri upigwaji wa muziki wa Nigeria nchini kwao kuliko hata muziki wa nchi yao na hata mataifa mengine.

“Nimekuwa nikiingia kwenye kumbi nyingi za Kinigeria nchini Marekani na wanacheza asilimia 95 Muziki wa Nigeria. Na nimewahi kuingia kwenye kumbi za wa Cameroon, moja niliingia usiku wa jana baada ya onesho langu, nilikuwa na marafiki. Tulikuwa wote wa Cameroon na zilitumika kama Ksh. 2M, licha ya matumizi yote hayo, ulisikika muziki wa Nigeria tu usiku mzima pale club kwa asilimia 70. Ni kwamba tumekosa uzalendo au ni hatuna nyimbo nzuri za Cameroon kwa ajili ya kuziomba club?” aliandika Mwanamuziki huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke