Msanii Innocent Balume maarufu kama ‘ Innoss’B ‘ kutoka nchini Congo DRC ameachia rasmi album yake mpya iitwayo ” Mortel-06 ” ambayo ina jumla ya ngoma 15.
Album hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kupitia majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani, haina collabo hata moja, kwani ngoma zote Innoss’B kapita nazo mwenyewe.
Mortel-06 album ina nyimbo kama Adieu, Boutchou, Toc toc,Eh Dieu, Sukali, Kweli, Minami, Mortel-06 na nyingine kibao.
Hii ni album ya tatu kutoka kwa mtu mzima Innoss’B baada ya Plus ya mwaka wa 2017 na Innocent ya mwaka wa 2013