Mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo TshalaMuana amefariki dunia leo Jumamosi, Disemba 10 mjini Kinshasa.
Mwenza wake aitwaye Claude Mashala amethibitisha taarifa za Kifo cha Mwanamuziki huyo kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Kwenye post hiyo, Mashala hajatoa sababu za Kifo cha Tshala Muana ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 64.
“Mapema asubuhi ya leo, Bwana mwema alichukua uamuzi wa kumchukua Mama wa Taifa Tshala Muana. Mungu mwema atukuzwe kwa nyakati zote njema alizotujalia hapa duniani. Kwaheri Mama kutoka kwa M,”ameandika Mashala.
Marehemu Tshala Muana alipata umaarufu barani Afrika kwa nyimbo kadhaa zilizovuma kila pembe sambamba na mtindo wa Mutuashi.
Nyimbo “Dezo Dezo” ya Ndala Kasheba na nyingine za Kiswahili ya “Karibu yangu”, “Tshibola” na nyingine zilimpa umaarufu sana Tanzania ambako alizuru mara kadhaa miaka ya 80 na 90