Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Ringtone ametoa changomoto kwa wasanii wenzake kutotegemea waandaji wa matamasha kwa ajili ya kupata shoo za kuingizia kipato.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni ringtone amewataka wasanii nchini kutumia umaarufu wao kwa kuja na shoo zao wenyewe watakazofanya maeneo mbali mbali nchini kama njia ya kujikwamua kiuchumi.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pamela” amesema wakenya wana moyo wa kuwasaidia wasanii wao lakini majivuno na kiburi imewaponza wasanii wengi na hivyo kuwafanya kukosa ubunifu wa kugeuza muziki wao kuwa biashara.
Utakumbuka mwaka wa 2010 Ringtone alianzisha mpango wa kutembelea shule zote za upili nchini kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wanafunzi kuhusu masuala yanayowaathiri ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwapa burudani na kuuza kanda za nyimbo zake jambo ambalo lilimuingizia pesa nyingi.