Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ray G, ametangaza kumpoteza binti yake Kim aliyekuwa na umri wa siku 12.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Ray G , amesema mtoto huyo alifariki Disemba 21 kufuatia kusumbuliwa na ugumu wa kupumua.
Msanii huyo amedokeza kwamba walifanya kila kitu kuokoa maisha ya binti yake huyo lakini juhudi zao ziliambuliwa patupu.
Kim alikuwa mtoto wa pili kwa Ray G na alimpata na mrembo Annabell Twinomugisha.