Msanii Weasel amefunguka anachokikosa kwa aliyekuwa mshirika wake kimuziki marehemu Mowzey Radio.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema kando na muziki huwa anaumia sana akimkumbuka maisha ya Radio kipindi cha uhai wake kwani walipenda sana kula bata pamoja kwenye maeneo mbali mbali ya burudani Jijini Kampala.
Msanii huyo amesema ikitokea amemjua aliyehusika na mauji ya Radio hatokuja kulipiza kisasi kwani ameamua kusahau kila kitu kama njia ya kupona na maumivu aliyoyapata kutokana na kifo cha msanii huyo.
Utakumbuka Mozey Radio alifariki dunia Februari 1 mwaka wa 2018 katika hospitali ya Case nchini Uganda kufuatia majeraha mabaya aliyoyapata alipovamiwa na mlinzi wa eneo moja la burudani viungani mwa jiji la Kampala.