Msanii kutoka nchini Kenya Xenia Manasseh ameachia rasmi Extended Playlist (EP) yake mpya iitwayo ” Maybe ” ambayo ina jumla ya ngoma 5.
EP hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kupitia majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani, haina collabo hata moja, kwani ngoma zote Xenia Manasseh kapita nazo mwenyewe.
Maybe EP ina nyimbo kama Etoile, Love Me or Leave Me, Lost, Maybe, na Circadian Riddim.
Hii ni EP ya pili kwa Xenia Manasseh baada ya Falling Apart iliyotoka mwaka wa 2020 ikiwa na jumla nyimbo 4 za moto.