You are currently viewing MWIGIZAJI BRUCE WILLIS ASTAAFU FILAMU KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA

MWIGIZAJI BRUCE WILLIS ASTAAFU FILAMU KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA

Mwigizaji gwiji wa filamu nchini Marekani Bruce Willis amestaafu baada ya kubainika kuwa na Aphasia, ambayo ni changamoto ya matamshi inayosababishwa na ubongo kuwa na tatizo linaloathiri uwezo wa mtu kuwasiliana.

Taarifa iliyotolewa na familia yake imesema baada ya kutafakari kwa muda Bruce  ameamua kuachana na tasnia hiyo ambayo ina maana kubwa sana kwake.

Utakumbuka Bruce Willis mwenye umri wa miaka 67 alianza uigizaji mwanzoni mwa miaka ya 1970, na nyota yake iling’aa na kuanza kutambulia kutokana na ushiriki wake mkuu katika filamu Za Moonlight, American Siege, Hostage, Hard Kill na nyingine kali takribani 125.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke