Mwigizaji Joseph Kinuthia maarufu kama Omosh amepuzilia mbali madai yanayotembea mtandaoni kuwa ana msongo wa mawazo baada ya familia yake kumkimbia.
Kupitia video aliyopakia kwenye mtandao wa youtubemwigizaji wa zamani wa Tahidi High amesema madai hayo hayana msingi wowote huku akitoa angalizo kwa wakenya kutoamini wanachokiano mitandaoni kwani anaendelea vizuri na maisha yake ya kawaida bila tatizo lolote.
Mwigizaji huuyo amewataka wanablogu kukoma kumchafulia jina mtandaoni kwa kumzushia taarifa za uongo kwa lengo la kupata idadi kubwa ya watazamaji kwenye mtandao wa youtube
Hata hivyo amewaondolea hofu mashabiki zake kwa kuwaahidi kuwa atarejea kwenye faini ya uigizaji hivi karibuni kwani ukimya wake umetokana na yeye kujikita zaidi kwenye utayarishaji wa kazi za filamu.
Kauli ya Omosh imekuja siku moja baada ya mwimbaji Akothee kutaka kujua hali ya mwigizaji huyo kufuatia taarifa iliyosambaa mtandaoni kuwa amepatwa na msongo wa mawazo baada ya wake zake wawili kumkimbia alipofilisika kiuchumi.