You are currently viewing Mwigizaji maarufu wa vichekesho Gibson Gathu afariki dunia

Mwigizaji maarufu wa vichekesho Gibson Gathu afariki dunia

Mwigizaji maarufu wa vichekesho wa kipindi cha “Vioja Mahakamani” kinachorushwa na runinga ya KBC cha Kenya Gibson Gathu Mbugua, almaarufu ‘Kiongozi wa Mashtaka’, amefariki dunia

Familia ya Gibson imeeleza kuwa mchekeshaji huyo amefariki dunia leo Alhamisi, Desemba 22 akiwa katika Hospitali ya Mediheal, mjini Eldoret ambako alikuwa akipokea matibabu.

Gibson Mbugua alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa zaidi ya miaka 20 na baadae alipata shida kwenye figo ambapo aliandaa harambee ya kumchangia gharama za upasuaji wa figo

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke