You are currently viewing MWIIMBAJI MWENYE UTATA NCHINI JUSTINA SYOKAU AWAONYA WANAUME WANAOMTAKA KIMAPENZI

MWIIMBAJI MWENYE UTATA NCHINI JUSTINA SYOKAU AWAONYA WANAUME WANAOMTAKA KIMAPENZI

Msanii wa nyimbo za Injili mwenye utata nchini Justina Syokau anaendelea kushika headlines za habari za burudani nchini na vituko vyake.

Katika mahojiano yake ya hivi karibu na runinga ya Ntv, hitmaker huyo twenty twenty ametoa onyo kali kwa wanaume ambao kwa njia moja au nyingine wamefulia kiuchumi wasijaribu kumtokea kimapenzi.

Kwa mujibu wa msanii huyo mwanaume ndiye anafaa kuwa mtoa riziki kwa familia na sio mwanamke huku akiongeza kuwa mwanaume yeyote anayemtegemea mwanamke kulishwa ni mtu mvivu ambaye hatakikani kwa ulimwengu wa sasa.

Mwanamama huyo ameenda mbali zaidi na kujitapa kuwa atakuwa anazungumza tu na wanaume wanaoendesha magari makubwa kama Mercedes benz na wanaume wanaomiliki ndege aina ya helicopter.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kukerwa na matamshi ya Justina Syokau ambapo wamemtaka msanii huyo aelekeze nguvu zake kwenye suala la kutoa muziki mzuri badala ya kulazimisha azungumzie kwenye vyombo vya habari wakati nyimbo zake ni mbovu

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke