You are currently viewing MWIMBAJI NYOTA WA WIMBO “EKWUEME” AFARIKI DUNIA

MWIMBAJI NYOTA WA WIMBO “EKWUEME” AFARIKI DUNIA

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria aitwaye Sister Osinachi Nwachukwu maarufu kwa wimbo wake “Ekwueme” amefariki dunia katika Hospitali moja iliyoko Abuja nchini Nigeria.

Osinachi alifariki dunia jioni ya jana Ijumaa (April 8, 2022) baada ya Kupambana na ugonjwa usiojulikana kwa takriban miezi miwili huku vyanzo vingine vikidai ni kansa ya koo

Kifo cha Osinachi kinakuja ikiwa ni wiki mbili tu tangu kifo cha mwimbaji mwenzake Chinedu Nwadike.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 39 alidaiwa kuwa anaendelea vizuri kutokana na maradhi ya figo na alikuwa amepangiwa kusafirishwa kwenda nchini India kwa matibabu zaidi ambapo kifo chake kilimkuta Machi 27, 2022 kabla hajaondoka kwenda India kutibiwa.

Baadhi yake nyimbo za Osinachi pamoja na “Nara Ekele” akiwa na Mchungaji Paul Enenche (Dunamis, Abuja), “Ekwueme” akiwa na Prospa Ochimana na nyinginezo nyingi zinazopendwa na kusikiliza/kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.

Wimbo wa Ekwueme umejipatia umaarufu sana kutokana maudhui yake huku ukitasambaa na kuimbwa na jamii kubwa duniani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke