You are currently viewing Mwimbaji wa Marekani Matt B adokeza kufanya kolabo na Bebe Cool

Mwimbaji wa Marekani Matt B adokeza kufanya kolabo na Bebe Cool

Msanii kutoka  Marekani Matt B amefichua mpango wa kufanya kazi  ya pamoja na wasanii wa Uganda.

Kupiti ukurasa wake wa Instagram amemtaja Bebe Cool kama mmoja wa wasanii ambao huenda akafanya nao kazi ambapo alienda mbali zaidi na kuwauliza mashabiki namna wimbo wao utakavyosikika masikioni mwao.

“Nilipata nafasi ya kukutana na Bebe Cool ilikuwa heshima. Nashangaa namna wimbo wa Bebe Cool na Matt B utasikika,” aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Utakumbuka Matt B ni moja kati ya wasanii walioteuliwa kushiriki tuzo za Grammy 2023 kupitia Wimbo wake na Eddy Kenzo “Gimme Love”.

Wawili hao waliotajwa kuwania kipengele cha Best Global Music Performance wanatarajiwa kuchuana na wasanii Burna Boy, Rocky Dawuni na Blvk H3ro, na Bayethe Wouter Kellerman, Zakes Bantwini na Nomcebo Zikode.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke