Mwimbaji wa nyimbo za injili Aniset Butati ameachia Extended Playlist (EP) yake mpya iitwayo “Take Over” yenye jumla ya nyimbo saba.
Ep hiyo ambayo ni ya kwanza katika safari ya muziki ya Aniset Butati ina nyimbo kama “Take Over”, ” Ni wewe”, “Waite”, ” Waone”, “Siwezi”, ” Mwema” na “Hakuna Kama Wewe”.
Aidha, Take Over EP tayari inapatikana kupitia digital platforms zote na miongoni mwa watayarishaji waliohusika kuitayarisha Ep hiyo ni pamoja na Mocco Genius na Man Walter.