Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili kutoka nchini Nigeria, Sammie Okposo amefariki dunia.
Kulingana na ripoti, Okposo mwenye umri wa miaka 51 alianguka na kufariki Ijumaa asubuhi.
Kifo chake ” kinakuja miezi kadhaa baada ya kukumbwa na kashfa ya uzinzi.
Mwimbaji huyo wa ‘Wellu Wellu’, katika ukurasa wa Instagram, aliwataka Wanigeria kumuombea.
Alikiri kudanganya mke wake aliposafiri kwenda Marekani mwishoni mwa 2021.
Sammie Okposo pia alisimamisha huduma yake hadi atakapopata kibali tena huku akiomba msamaha kutoka kwa Mungu.