Mwanamuziki wa nyimbo za injili Master Piece amejibu wanaodai kuwa ameacha muziki wa injili kimya kimya na kugeukia uimbaji nyimbo za kiduani kwa lengo la kujitafutia pesa.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Master Piece amewataka walimwengu waache tabia ya kuwakosoa wasanii na badala yake wasapoti muziki mzuri wanaoufanya kama njia ya kutangaza muziki wa Kenya kimataifa.
Msanii huyo amesema kuimba nyimbo za mapenzi sio dhambi kama watu wengi wanavyodhani na kusisitiza kuwa ni suala ambalo lipo kwenye maandiko matakatifu, hivyo haoni umuhimu wa watu kutilia shaka uimbaji wake kwa kuwa bado anamtumikia Mungu.
Katika hatua nyingine Master Piece amemtolea uvivu msanii Willy Paul kwa kusema kwamba msanii huyo aliishusha brand yake ya muziki alipoamua kununua gari aina ya matatu kwani haeindani na kiwango cha maisha anayoishi kwa sasa.
Hata hivyo amezungumzia suala la kutaka kumpeleka kanisani Mrembo Huddah Monroe kwa kusema kuwa hakuwa na nia ya kumchumbia mrembo huyo kimahaba bali alitaka kumtumia kubadilisha maisha ya vijana wengi kupitia umaarufu alionao kwa jamii ili waweze kukumbatia uwokovu.