You are currently viewing Mwimbaji William Getumbe akanusha kutumia suala la kukojoa kitandani kutafuta kiki

Mwimbaji William Getumbe akanusha kutumia suala la kukojoa kitandani kutafuta kiki

Mwanamuziki wa injili kutoka Eldoret William Getumbe amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya kutumia suala la kukojoa kitandani kutafuta kiki.

Kwenye mahojiano na Nicholas Kioko, Getumbe amekanusha madai ya kutumia hali yake kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni huku akisema kuwa aliamua kuweka wazi masaibu yake kwa umma kwa ajili ya kuondoa mitazamo hasi kwa watu wanaokojoa kitandani.

Bosi huyo wa Billgates Records amesema amekuwa akikumbana na tatizo hilo kwa kipindi cha miaka minne sasa, jambo ambalo limempelekea kuvalia nepi kama njia ya kuepuka aibu katika jamii.

Hata hivyo Getumbe mwenye umri wa miaka 48 amewataka wanaume wanaopitia hali kama yake kutojificha na badala yake wawashirikishe wake zao ili kuzuia migogoro kwenye ndoa.

Kauli yake imekuja mara baada ya kukiri kwenye mahojiano na Tuko kwamba amekuwa akikojoa kitandani akiwa kwenye ndoa ambapo alienda mali zaidi na kusema kuwa mke wake Virginia Masitha, amekuwa akimvisha nepi nyakati za usiku, kumuepusha kulowesha malazi yao kwa mkojo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke