You are currently viewing NAAVA THE QUEEN APUZILIA MBALI TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA WANASIASA

NAAVA THE QUEEN APUZILIA MBALI TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA WANASIASA

Mwigizaji kutoka Kenya Naava The Queen amepuzilia mbali madai ya kutembea kimapenzi na wanasiasa.

Hii ni baada ya walimwengu kuhoji kuwa maisha ya kifahari anayoonesha mtandaoni yanafadhiliwa na wanasiasa ambao amekuwa akitoka nao kimapenzi.

Sasa kwenye mahojiano yake mapya Naava The Queen amezima tetesi hizo kwa kusema kwamba hayana msingi wowote kwani maisha ya kifahari anayoishi ni kutokana na yeye kujituma zaidi kwenye shughuli zake za uigizaji.

Katika hatua nyingine mrembo huyo alipata umaarufu mkubwa kwenye vipindi vya runinga nchini amekanusha madai ya kufanyia mwili wake surgery ili kuboresha muonekano wake kwa kusema kuwa hajawahi jihusisha na vitendo vya kubadili muonekano wake kwa njia ya upasuaji.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke